Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hafla hiyo imefanyika chini ya usimamizi wa Maulana Sheikh Hemed Jalala, Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithnaasharia Tanzania (TIC), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ambayo huwaleta pamoja waumini katika mazingira ya ibada, mapenzi na kumuenzi Mtume wa Allah (s.a.w.w.).
Katika hafla hiyo, Madrasa ya Maawa Islamiya Kutoka Tanga, ilialikwa na kushiriki kuongoza zoezi la Samāi, likiwa ni miongoni mwa shughuli zinazolenga kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na kuimarisha mapenzi na mshikamano miongoni mwa Waislamu.
Maadhimisho hayo yanaendelea leo kupitia hafla kubwa ya Maulidi ya Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.), itakayofanyika katika viwanja vya Pipo, Kigogo, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 22:00 usiku. Hafla hiyo inatarajiwa kuwa fursa muhimu ya waumini kukutana kwa ajili ya kumuenzi Mtume (s.a.w.w.), kusikiliza mawaidha na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kumbukumbu ya Maulidi.
Waumini wote na wananchi kwa ujumla mnakaribishwa kushiriki katika hafla hii adhimu ya kumuenzi Mtume Mtukufu Muhammad (s.a.w.w.).





Maoni yako